Zaburi 119:9-16
Zaburi 119:9-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Kijana atatunzaje maisha yake kuwa safi? Kwa kuyaongoza kadiri ya neno lako. Najitahidi kukutii kwa moyo wote; usiniache nikiuke amri zako. Nimeshika neno lako moyoni mwangu, nisije nikakukosea. Utukuzwe, ee Mwenyezi-Mungu! Unifundishe masharti yako. Nitayarudia kwa sauti maagizo yako yote uliyotoa. Nafurahi kufuata maamuzi yako, kuliko kuwa na utajiri mwingi. Nazitafakari kanuni zako, na kuzizingatia njia zako. Nayafurahia masharti yako; sitalisahau neno lako.
Zaburi 119:9-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako. Kwa midomo yangu nimezisimulia Hukumu zote za kinywa chako. Nimeifurahia njia ya shuhuda zako Kana kwamba ni mali mengi. Nitayatafakari maagizo yako, Na kuziangalia njia zako. Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.
Zaburi 119:9-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako. Kwa midomo yangu nimezisimulia Hukumu zote za kinywa chako. Nimeifurahia njia ya shuhuda zako Kana kwamba ni mali mengi. Nitayatafakari mausia yako, Nami nitaziangalia njia zako. Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.
Zaburi 119:9-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako. Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako. Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi. Sifa ni zako, Ee BWANA, nifundishe maagizo yako. Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako. Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi. Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako. Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako.