Zaburi 119:86-88
Zaburi 119:86-88 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maagizo yako yote ni amini, Wananifuatia bure, unisaidie. Walikuwa karibu na kunikomesha katika nchi, Lakini sikuyaacha mausia yako. Unihuishe kwa fadhili zako, Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.
Zaburi 119:86-88 Biblia Habari Njema (BHN)
Amri zako zote ni za kuaminika; watu wananitesa bila haki; unisaidie! Karibu wangefaulu kuniangamiza, lakini mimi sijavunja kanuni zako. Unisalimishe kadiri ya fadhili zako, nipate kuzingatia maamuzi uliyotamka.
Zaburi 119:86-88 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Amri zako zote ni za kudumu, Ninateswa bila sababu, nisaidie! Walikuwa karibu na kunikomesha katika nchi, Lakini sikuyaacha mausia yako. Uniponye kwa fadhili zako, Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.
Zaburi 119:86-88 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maagizo yako yote ni amini, Wananifuatia bure, unisaidie. Walikuwa karibu na kunikomesha katika nchi, Lakini sikuyaacha mausia yako. Unihuishe kwa fadhili zako, Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.
Zaburi 119:86-88 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Amri zako zote ni za kuaminika; unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu. Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, lakini sijaacha mausia yako. Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, nami nitatii sheria za kinywa chako.