Zaburi 119:83-85
Zaburi 119:83-85 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, bado sijasahau maagizo yako. Mtumishi wako itampasa angoje hadi lini? Ni lini utawaadhibu washtaki wangu? Wenye majivuno wananichimbia mashimo, kinyume na sheria yako.
Shirikisha
Soma Zaburi 119Zaburi 119:83-85 Biblia Habari Njema (BHN)
Nimekunjamana kama kiriba katika moshi, hata hivyo sijasahau masharti yako. Mimi mtumishi wako nitasubiri mpaka lini? Utawaadhibu lini wale wanaonidhulumu? Wenye kiburi wamenichimbia mashimo, watu ambao hawafuati sheria yako.
Shirikisha
Soma Zaburi 119Zaburi 119:83-85 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana nimekuwa kama kiriba katika moshi, Sikuzisahau amri zako. Siku za mtumishi wako ni ngapi, Lini utakapowahukumu wale wanaonifuatia? Wenye kiburi wamenichimbia mashimo, Ambao hawaifuati sheria yako.
Shirikisha
Soma Zaburi 119