Zaburi 119:53-56
Zaburi 119:53-56 Biblia Habari Njema (BHN)
Nashikwa na hasira kali, nionapo waovu wakivunja sheria yako. Masharti yako yamekuwa wimbo wangu, nikiwa huku ugenini. Usiku ninakukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, na kushika sheria yako. Hii ni baraka kubwa kwangu, kwamba nazishika kanuni zako.
Zaburi 119:53-56 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ghadhabu kuu imenishika kwa sababu ya wasio haki, Waiachao sheria yako. Amri zako zimekuwa nyimbo zangu, Katika nyumba yangu ya ugenini. Wakati wa usiku nimelikumbuka jina lako, Ee BWANA, nikaitii sheria yako. Hayo ndiyo niliyokuwa nayo, Kwa sababu nimeyashika mausia yako.
Zaburi 119:53-56 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ghadhabu imenishika kwa sababu ya wasio haki, Waiachao sheria yako. Amri zako zimekuwa nyimbo zangu, Katika nyumba ya ugeni wangu. Wakati wa usiku nimelikumbuka jina lako, Ee BWANA, nikaitii sheria yako. Hayo ndiyo niliyokuwa nayo, Kwa sababu nimeyashika mausia yako.
Zaburi 119:53-56 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, ambao wameacha sheria yako. Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu popote ninapoishi. Ee Mwenyezi Mungu, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, nami nitatii sheria yako. Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako.