Zaburi 119:41-48
Zaburi 119:41-48 Biblia Habari Njema (BHN)
Fadhili zako zinijie, ee Mwenyezi-Mungu; uniokoe kama ulivyoahidi. Hapo nitaweza kuwajibu hao wanaonitukana, maana mimi nina imani sana na neno lako. Unijalie kusema ukweli wako daima, maana tumaini langu liko katika maagizo yako. Nitatii sheria yako daima, nitaishika milele na milele. Nitaishi katika uhuru kamili, maana nazitilia maanani kanuni zako. Nitawatangazia wafalme maamuzi yako, wala sitaona aibu. Furaha yangu ni kuzitii amri zako, ambazo mimi nazipenda. Naziheshimu na kuzipenda amri zako; nitayatafakari masharti yako.
Zaburi 119:41-48 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, fadhili zako zinifikie na mimi, Naam, wokovu wako kulingana na ahadi yako. Nami nitamjibu neno anilaumuye, Kwa maana nilitumainia neno lako. Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, Maana nimezingojea hukumu zako. Nami nitaitii sheria yako daima, Naam, milele na milele. Nami nitakwenda kwa uhuru, Kwa kuwa nimejifunza mausia yako. Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu. Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda. Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari amri zako.
Zaburi 119:41-48 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, fadhili zako zinifikie na mimi, Naam, wokovu wako sawasawa na ahadi yako. Nami nitamjibu neno anilaumuye, Kwa maana nalitumainia neno lako. Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, Maana nimezingojea hukumu zako. Nami nitaitii sheria yako daima, Naam, milele na milele. Nami nitakwenda panapo nafasi, Kwa kuwa nimejifunza mausia yako. Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu. Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda. Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari amri zako.
Zaburi 119:41-48 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako, ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako. Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako. Nitaitii amri yako daima, naam, milele na milele. Nitatembea nikiwa huru, kwa kuwa nimejifunza mausia yako. Nitasema sheria zako mbele za wafalme wala sitaaibishwa, kwa kuwa ninazifurahia amri zako kwa sababu ninazipenda. Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu, nami ninatafakari juu ya maagizo yako.