Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 119:107-109 - Compare All Versions

Zaburi 119:107-109 BHN (Biblia Habari Njema)

Ee Mwenyezi-Mungu, ninateseka mno; unijalie uhai kama ulivyoahidi. Ee Mwenyezi-Mungu, upokee sala yangu ya shukrani; na kunifundisha maagizo yako. Maisha yangu yamo hatarini daima, lakini siisahau sheria yako.

Shirikisha
Zaburi 119 BHN

Zaburi 119:107-109 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Nimeteswa mno; Ee BWANA, unihuishe sawasawa na neno lako. Ee BWANA, uziridhie sadaka za kinywa changu, Na kunifundisha hukumu zako. Nafsi yangu imo mkononi mwangu daima, Lakini sheria yako sikuisahau.

Shirikisha
Zaburi 119 SUV

Zaburi 119:107-109 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Nimeteswa mno; Ee BWANA, unihuishe sawasawa na neno lako. Ee BWANA, uziridhie sadaka za kinywa changu, Na kunifundisha hukumu zako. Nafsi yangu imo mkononi mwangu daima, Lakini sheria yako sikuisahau.

Shirikisha
Zaburi 119 SRUV

Zaburi 119:107-109 NEN (Neno)

Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee BWANA, sawasawa na neno lako. Ee BWANA, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako. Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, sitasahau sheria yako.

Shirikisha
Zaburi 119 NEN