Zaburi 119:102-104
Zaburi 119:102-104 Biblia Habari Njema (BHN)
Sikukiuka maagizo yako, maana wewe mwenyewe ulinifundisha. Maneno yako ni matamu sana kwangu; naam, ni matamu kuliko asali! Kwa kanuni zako napata hekima, kwa hiyo nachukia kila mwenendo mbaya.
Zaburi 119:102-104 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikuziacha hukumu zako, Maana Wewe mwenyewe umenifundisha. Mausia yako ni matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu. Kwa mausia yako najipatia ufahamu, Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
Zaburi 119:102-104 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sikujiepusha na hukumu zako, Maana Wewe mwenyewe umenifundisha. Mausia yako ni matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu. Kwa mausia yako najipatia ufahamu, Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
Zaburi 119:102-104 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe. Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu! Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.