Zaburi 112:1-3
Zaburi 112:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake. Wazawa wake watakuwa wenye nguvu nchini; watoto wa wanyofu watapata baraka. Nyumbani kwake kutakuwa na mali nyingi; uadilifu wake wadumu milele.
Zaburi 112:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake. Wazawa wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yadumu milele.
Zaburi 112:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake. Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele.
Zaburi 112:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Msifuni BWANA. Heri mtu yule amchaye BWANA, mtu yule apendezwaye sana na amri zake. Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. Nyumbani mwake kuna mali na utajiri, haki yake hudumu milele.