Zaburi 108:1-6
Zaburi 108:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Niko thabiti moyoni, ee Mungu, naam, niko thabiti moyoni; nitaimba na kukushangilia! Amka, ee nafsi yangu! Amkeni enyi kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko! Ee Mwenyezi-Mungu, nitakushukuru kati ya mataifa; nitakuimbia sifa kati ya mataifa. Fadhili zako ni kubwa kuliko mbingu; uaminifu wako waenea hata mawinguni. Utukuzwe, ee Mungu juu ya mbingu! Utukufu wako uenee duniani kote! Watu hao uwapendao na wasalimishwe; utusaidie kwa mkono wako na kutusikiliza.
Zaburi 108:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Nitaimba, nitaimba zaburi, Naam, kwa utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri. Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia sifa kati ya mataifa. Maana fadhili zako ni kubwa kuliko mbingu, Na uaminifu wako unafika hata mawinguni. Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako. Ili watu uwapendao waokolewe, 2 Unipe ushindi kwa mkono wako wa kulia, na uniitikie.
Zaburi 108:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Nitaimba, nitaimba zaburi, Naam, kwa utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri. Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa. Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni. Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako. Ili wapenzi wako waopolewe, Uokoe kwa mkono wako wa kuume, uniitikie.
Zaburi 108:1-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. Nitakusifu wewe, Ee BWANA, kati ya mataifa; nitaimba habari zako, katika jamaa za watu. Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu; uaminifu wako unazifikia anga. Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale unaowapenda wapate kuokolewa.