Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 108

108
Sifa na sala ya ushindi
Wimbo. Zaburi ya Daudi.
1Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,
Nitaimba, nitaimba zaburi,
Naam, kwa utukufu wangu.
2Amka, kinanda na kinubi,
Nitaamka alfajiri.
3Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu,
Nitakuimbia sifa kati ya mataifa.
4 # Mik 7:18-20; Hes 14:18; Kum 7:9; Zab 36:5 Maana fadhili zako ni kubwa kuliko mbingu,
Na uaminifu wako unafika hata mawinguni.
5 # Zab 57:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6Ili watu uwapendao waokolewe,
2 Unipe ushindi kwa mkono wako wa kulia, na uniitikie.
7Mungu amenena kwa utakatifu wake,
Nami nitashangilia.
Nitaigawanya Shekemu,
Nitalipima bonde la Sukothi.
8 # Mwa 49:10; Zab 60:7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,
Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu.
Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,
9Moabu ni bakuli langu la kunawia.
Nitamtupia Edomu kiatu changu,
Na kumpigia Filisti kelele za vita.
10 # Zab 60:9 Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye boma?
Ni nani atakayeniongoza hadi Edomu?
11Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?
Wala, Ee Mungu, huendi na majeshi yetu?
12Utuletee msaada juu ya mtesi,
Maana wokovu wa binadamu haufai.
13 # Isa 25:10; 30:3; Omb 1:15; Mal 4:3; Mdo 1:20; Ufu 14:19-20 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,
Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 108: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha