Zaburi 103:8-10
Zaburi 103:8-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu ni mwenye rehema na huruma; ni mvumilivu na mwingi wa fadhili. Hatukemeikemei daima, wala hasira yake haidumu milele. Yeye hatuadhibu kama tunavyostahili; hatulipizi kadiri ya uovu wetu.
Zaburi 103:8-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Yeye hatashutumu daima, Wala hatashika hasira yake milele. Hakututenda kulingana na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
Zaburi 103:8-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Yeye hatateta sikuzote, Wala hatashika hasira yake milele. Hakututenda sawasawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
Zaburi 103:8-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo. Yeye hatalaumu siku zote, wala haweki hasira yake milele, yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.