Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 103

103
Sala kuu ya shukrani
(Zaburi ya Daudi)
1Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu;
nafsi yangu yote ilisifu jina lake takatifu!
2Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu!
Usisahau kamwe wema wake wote.
3Ndiye anayenisamehe uovu wangu wote,
na kuniponya magonjwa yote.
4Ndiye aniokoaye kutoka kifoni,
na kunijalia rehema na fadhili zake.
5Ndiye anayeniridhisha mema maisha yangu yote,
hata nabaki kijana mwenye nguvu kama tai.
6Mwenyezi-Mungu huhukumu kwa haki;
huwajalia wanaodhulumiwa haki zao.
7Alimjulisha Mose mwongozo wake,
aliwaonesha watu wa Israeli matendo yake.
8Mwenyezi-Mungu ni mwenye rehema na huruma;
ni mvumilivu na mwingi wa fadhili.
9Hatukemeikemei daima,
wala hasira yake haidumu milele.
10Yeye hatuadhibu kama tunavyostahili;
hatulipizi kadiri ya uovu wetu.
11Kama vile anga lilivyo juu mbali na dunia,
ndivyo ulivyo mwingi wema wake kwa watu wanaomcha.
12Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
ndivyo azitengavyo dhambi zetu mbali nasi.
13Kama vile baba amhurumiavyo mwanawe,
ndivyo Mwenyezi-Mungu awahurumiavyo wote wamchao.
14Mungu ajua mfumo wa nafsi zetu;
ajua kwamba sisi ni mavumbi.
15Walakini binadamu, maisha yake ni kama nyasi tu;
huchanua kama ua shambani:
16Upepo huvuma juu yake nalo latoweka;
na mahali lilipokuwa hapaonekani tena.
17Lakini fadhili za Mwenyezi-Mungu hudumu milele,
kwa wale wote wanaomheshimu;
na wema wake wadumu vizazi vyote,
18kwa wote wanaozingatia agano lake,
wanaokumbuka kutii amri zake.
19Mwenyezi-Mungu ameweka kiti chake cha enzi mbinguni;
yeye anatawala juu ya vitu vyote.
20Enyi malaika wakuu, msifuni Mwenyezi-Mungu;
mnaotimiza amri zake na kutekeleza neno lake!
21Enyi jeshi lote la mbinguni, msifuni Mwenyezi-Mungu;
enyi watumishi wake mnaotekeleza matakwa yake!
22Msifuni Mwenyezi-Mungu enyi viumbe vyake vyote;
msifuni popote mlipo katika milki yake.
Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu!

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 103: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha