Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 103:11-12 - Linganisha Matoleo Yote

Zaburi 103:11-12 BHN (Biblia Habari Njema)

Kama vile anga lilivyo juu mbali na dunia, ndivyo ulivyo mwingi wema wake kwa watu wanaomcha. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo azitengavyo dhambi zetu mbali nasi.

Shirikisha
Zaburi 103 BHN

Zaburi 103:11-12 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

Shirikisha
Zaburi 103 SUV

Zaburi 103:11-12 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

Shirikisha
Zaburi 103 SRUV

Zaburi 103:11-12 NEN (Neno)

Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia, ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha; kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.

Shirikisha
Zaburi 103 NEN