Zaburi 103:1-8
Zaburi 103:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu; nafsi yangu yote ilisifu jina lake takatifu! Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! Usisahau kamwe wema wake wote. Ndiye anayenisamehe uovu wangu wote, na kuniponya magonjwa yote. Ndiye aniokoaye kutoka kifoni, na kunijalia rehema na fadhili zake. Ndiye anayeniridhisha mema maisha yangu yote, hata nabaki kijana mwenye nguvu kama tai. Mwenyezi-Mungu huhukumu kwa haki; huwajalia wanaodhulumiwa haki zao. Alimjulisha Mose mwongozo wake, aliwaonesha watu wa Israeli matendo yake. Mwenyezi-Mungu ni mwenye rehema na huruma; ni mvumilivu na mwingi wa fadhili.
Zaburi 103:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako kutoka kwa kaburi, Akutia taji la fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai; BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa. Alimjulisha Musa njia zake, Wana wa Israeli matendo yake. BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Zaburi 103:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai; BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa. Alimjulisha Musa njia zake, Wana wa Israeli matendo yake. BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Zaburi 103:1-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usisahau wema wake wote: akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akuvika taji la upendo na huruma, atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, ili ujana wako uhuishwe kama wa tai. BWANA hutenda haki, naye huwapa hukumu ya haki wote wanaodhulumiwa. Alimjulisha Musa njia zake, na watu wa Israeli matendo yake. BWANA ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.