Zaburi 101:1-3
Zaburi 101:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Utenzi wangu kuhusu uaminifu na haki; ninauimba kwa heshima yako, ee Mwenyezi-Mungu. Nitazingatia mwenendo usio na hatia. Je, utakuja kwangu lini? Nitaishi kwa unyofu nyumbani kwangu; sitavumilia kamwe upuuzi. Nayachukia matendo ya watu wapotovu, mambo yao hayataambatana nami.
Zaburi 101:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Rehema na hukumu nitaziimba, Ee BWANA, nitakuimbia zaburi. Nitakuwa na mwenendo usio na hatia; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu. Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.
Zaburi 101:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Rehema na hukumu nitaziimba, Ee BWANA, nitakuimbia zaburi. Nitaiangalia njia ya unyofu; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu. Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.
Zaburi 101:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nitaimba kuhusu upendo wako na haki yako; kwako wewe, Ee BWANA, nitaimba sifa. Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: utakuja kwangu lini? Nitatembea nyumbani mwangu kwa moyo usio na lawama. Sitaweka mbele ya macho yangu kitu kiovu.