Zaburi 1:3-4 - Compare All Versions
Zaburi 1:3-4 BHN (Biblia Habari Njema)
Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito, unaozaa matunda kwa wakati wake, na majani yake hayanyauki. Kila afanyalo hufanikiwa. Lakini waovu sivyo walivyo; wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
Zaburi 1:3-4 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
Zaburi 1:3-4 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
Zaburi 1:3-4 NEN (Neno)
Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa. Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yanayopeperushwa na upepo.