Methali 6:6-11
Methali 6:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi, fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima. Sisimizi hana kiongozi, ofisa, wala mtawala; lakini hujiwekea chakula wakati wa kiangazi, hujikusanyia akiba wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hapo mpaka lini? Utaamka lini katika usingizi wako? Wasema: “Acha nilale kidogo tu, acha nisinzie kidogo! Niache nikunje mikono nipumzike kidogo!” Wakati huo umaskini utakuvamia kama mnyanganyi, ufukara utakufuata kama jambazi.

Methali 6:6-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana kiongozi, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hadi lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Methali 6:6-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Methali 6:6-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima! Kwa maana yeye hana msimamizi, wala mwangalizi, au mtawala, lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaamka lini kutoka usingizi wako? Kulala kidogo, kusinzia kidogo, kukunja mikono kidogo upate kupumzika: umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.