Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 6

6
Mawaidha ya Vitendo
1 # Mwa 43:9; Mit 27:13; Ebr 7:22; Ezr 10:19 Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa rafiki yako,
Ikiwa wewe na mgeni mmepana mikono,
2Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako,
Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
3Sasa, mwanangu, fanya hivi ukajiokoe,
Kwa kuwa umejitia mkononi mwa jirani yako;
Nenda ukanyenyekee, na kumsihi jirani yako.
4 # Rut 3:18 Usiache macho yako kupata usingizi,
Wala kope za macho yako kusinzia.
5Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji,
Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.
6 # Ayu 12:7 Ewe mvivu, mwendee chungu,
Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7Kwa maana yeye hana akida,
Wala msimamizi, wala mkuu,
8Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;
Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
9Ewe mvivu, utalala hata lini?
Utaondoka lini katika usingizi wako?
10 # Mit 24:33-34 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
Bado kukunja mikono upate usingizi!
11Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi,
Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
12Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu;
Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu.
13 # Zab 35:19; Mit 10:10 Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu,
Huwaashiria watu kwa vidole vyake.
14 # Zab 36:4; Isa 32:7; Mik 2:1; Mt 26:4 Mna upotofu moyoni mwake, hutunga uovu daima,
Hupanda mbegu za magomvi.
15 # Yer 19:11 Basi msiba utampata kwa ghafula;
Ghafula atavunjika, bila njia ya kupona.
16Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA;
Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.
17 # Zab 5:6; Mit 12:22; Hos 4:1,2; Yn 8:44; Mit 1:11; Isa 1:15 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo,
Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18 # Mwa 6:5; Isa 59:7; Rum 3:15 Moyo uwazao mawazo mabaya;
Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;
19 # Zab 27:12 Shahidi wa uongo asemaye uongo;
Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
20 # Efe 6:1 Mwanangu, shika maagizo ya baba yako,
Wala usiiache sheria ya mama yako.
21Yafunge hayo katika moyo wako daima;
Jivike hayo shingoni mwako.
22Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda,
Na uamkapo yatazungumza nawe.
23 # Zab 19:8 Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru,
Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
24Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate,
Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.
25 # 2 Sam 11:2-5; Mt 5:28 Usiutamani uzuri wake moyoni mwako;
Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.
26 # Mit 29:3; Eze 13:18 Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate;
Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani
27Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake,
Na nguo zake zisiteketezwe?
28Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto,
Na nyayo zake zisiungue?
29Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake;
Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.
30Watu hawamdharau mwivi,
Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa;
31 # Kut 22:1,4 Lakini akipatikana, atalipa mara saba;
Atatoa mali yote ya nyumba yake.
32 # Ayu 31:12; Ebr 13:4 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
33Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;
Wala fedheha yake haitafutika.
34Maana wivu ni ghadhabu ya mtu;
Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.
35Hatakubali ukombozi uwao wote;
Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 6: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha