Methali 6:24-32
Methali 6:24-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Yatakulinda mbali na mwanamke mbaya, yatakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni. Usimtamani mwanamke huyo kwa uzuri wake, wala usikubali kunaswa kwa kope za macho yake. Mtu hupoteza kipande cha mkate kwa malaya, lakini kwa mke wa mtu mwingine utapoteza uhai wako wote. Je, waweza kuweka moto kifuani na nguo zako zisiungue? Je, waweza kukanyaga makaa ya moto na nyayo zako zisiungue? Ndivyo alivyo mwanamume alalaye na mke wa mwenzake; yeyote anayemgusa mwanamke huyo hataacha kuadhibiwa. Watu hawambezi sana mtu akiiba kwa sababu ya njaa; lakini akipatikana lazima alipe mara saba; tena atatoa mali yote aliyo nayo. Mwanamume anayezini na mke wa mtu hana akili kabisa; huyo hujiangamiza yeye mwenyewe.
Methali 6:24-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni. Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani Je! Mtu aweza kuchukua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe? Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue? Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia. Watu hawamdharau mwizi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa; Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake. Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Methali 6:24-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni. Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe? Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue? Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia. Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa; Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake. Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Methali 6:24-32 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka. Moyo wako usitamani uzuri wake, wala macho yake yasikuteke, kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini, hata ukose kipande cha mkate, naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa. Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake bila nguo zake kuungua? Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto bila miguu yake kuungua? Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine; hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa. Watu hawamdharau mwizi akiiba ili kukidhi njaa yake akiwa na njaa. Lakini akikamatwa, lazima alipe mara saba, ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake. Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa; yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.