Methali 6:23-29
Methali 6:23-29 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana amri hiyo ni taa, na sheria hiyo ni mwanga. Maonyo hayo na nidhamu yatuweka njiani mwa uhai. Yatakulinda mbali na mwanamke mbaya, yatakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni. Usimtamani mwanamke huyo kwa uzuri wake, wala usikubali kunaswa kwa kope za macho yake. Mtu hupoteza kipande cha mkate kwa malaya, lakini kwa mke wa mtu mwingine utapoteza uhai wako wote. Je, waweza kuweka moto kifuani na nguo zako zisiungue? Je, waweza kukanyaga makaa ya moto na nyayo zako zisiungue? Ndivyo alivyo mwanamume alalaye na mke wa mwenzake; yeyote anayemgusa mwanamke huyo hataacha kuadhibiwa.
Methali 6:23-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima. Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni. Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani Je! Mtu aweza kuchukua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe? Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue? Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.
Methali 6:23-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima. Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni. Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe? Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue? Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.
Methali 6:23-29 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa maana amri hii ni taa, mafundisho haya ni mwanga, na maonyo ya nidhamu ni njia ya uzima, yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka. Moyo wako usitamani uzuri wake, wala macho yake yasikuteke, kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini, hata ukose kipande cha mkate, naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa. Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake bila nguo zake kuungua? Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto bila miguu yake kuungua? Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine; hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.