Methali 3:3-5
Methali 3:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Utii na uaminifu visitengane nawe. Vifunge shingoni mwako; viandike moyoni mwako. Hivyo utakubalika na kusifika, mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu. Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe.
Methali 3:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe
Methali 3:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe
Methali 3:3-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako. Ndipo utapata kibali na jina zuri mbele za Mungu na mwanadamu. Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe