Methali 3:13-20
Methali 3:13-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Heri mtu anayegundua hekima, mtu yule anayepata ufahamu. Hekima ni bora kuliko fedha, ina faida kuliko dhahabu. Hekima ina thamani kuliko johari, hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo. Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu; kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima. Njia zake ni za kupendeza, zote zaelekea kwenye amani. Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao; wana heri wote wanaoshikamana naye. Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia, kwa akili aliziimarisha mbingu. Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka, na mawingu yakadondosha umande.
Methali 3:13-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani. Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu anayeshikamana naye. Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande.
Methali 3:13-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani. Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye. Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande.
Methali 3:13-20 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Heri mtu yule apataye hekima, mtu yule apataye ufahamu, kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi. Hekima ana thamani kuliko marijani; hakuna chochote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye. Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume; katika mkono wake wa kushoto kuna utajiri na heshima. Njia zake zinapendeza, mapito yake yote ni amani. Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; wale wamshikao watabarikiwa. Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya dunia, kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake; kwa maarifa yake vilindi viligawanywa, nayo mawingu yanadondosha umande.