Methali 3:1-3
Methali 3:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu, bali kwa moyo wako uzishike amri zangu. Maana yatakupa wingi wa siku, maisha marefu na fanaka kwa wingi. Utii na uaminifu visitengane nawe. Vifunge shingoni mwako; viandike moyoni mwako.
Methali 3:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani. Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
Methali 3:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani. Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
Methali 3:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako, kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio. Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako.