Methali 26:6-8
Methali 26:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Kumtuma mpumbavu ujumbe, ni kama kujikata miguu au kujitafutia shida. Methali mdomoni mwa mpumbavu, ni kama miguu ya kiwete inayoninginia. Kumpa mpumbavu heshima, ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo.
Methali 26:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu.
Methali 26:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu.
Methali 26:6-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa sumu, ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu. Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima.