Methali 26:6-12
Methali 26:6-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Kumtuma mpumbavu ujumbe, ni kama kujikata miguu au kujitafutia shida. Methali mdomoni mwa mpumbavu, ni kama miguu ya kiwete inayoninginia. Kumpa mpumbavu heshima, ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo. Mpumbavu anayejaribu kutumia methali, ni kama mlevi anayejaribu kungoa mwiba mkononi. Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi, ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu. Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake, ni kama mbwa anayekula matapishi yake. Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima? Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.
Methali 26:6-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu. Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao. Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena. Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Methali 26:6-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu. Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao. Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena. Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Methali 26:6-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa sumu, ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu. Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima. Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu. Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo, ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani. Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake. Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.