Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 26:1-16

Methali 26:1-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno, ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu. Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi, ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu! Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye. Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe. Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa sumu, ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu. Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima. Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu. Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo, ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani. Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake. Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake. Mvivu husema, “Yuko simba barabarani, simba mkali anazunguka mitaa!” Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake. Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.

Shirikisha
Soma Methali 26