Methali 25:7-17
Methali 25:7-17 Biblia Habari Njema (BHN)
maana ni heri kuambiwa, “Njoo huku mbele”, kuliko kuporomoshwa mbele ya mkuu. Mambo uliyoyaona kwa macho yako, usiharakishe kuyapeleka mahakamani; maana utafanya nini hapo baadaye, shahidi mwingine akibatilisha hayo usemayo? Suluhisha ugomvi na mwenzako peke yake, na kila mmoja wenu asitoe siri ya mwenzake; watu wasije wakajua kuna siri, ukajiharibia jina lako daima. Neno lisemwalo wakati unaofaa, ni kama nakshi za dhahabu juu ya madini ya fedha. Onyo la mwenye hekima kwa mtu msikivu, ni bora kuliko pete au vito vya dhahabu safi. Mjumbe mwaminifu humfurahisha yule aliyemtuma, kama maji baridi wakati wa joto la mavuno. Kama vile mawingu na upepo bila mvua, ndivyo alivyo mtu anayejigamba kutoa zawadi asiitoe. Kwa uvumilivu mtawala huweza kushawishika; ulimi laini huvunja mifupa. Upatapo asali kula kiasi cha kukutosha, usije ukaikinai na kuitapika. Usimtembelee jirani yako mara kwa mara, usije ukamchosha naye akakuchukia.
Methali 25:7-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho, Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha. Ujitetee na mwenzako peke yake; Bali usiifunue siri ya mtu mwingine; Yeye asikiaye asije akakutukana; Na aibu yako isiondoke. Neno linenwalo wakati ufaao, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha. Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo. Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao. Kama mawingu na upepo pasipo mvua; Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo. Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa. Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha; Usije ukashiba na kuitapika. Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; Asije akakukinai na kukuchukia.
Methali 25:7-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho, Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha. Ujitetee na mwenzako peke yake; Bali usiifunue siri ya mtu mwingine; Yeye asikiaye asije akakutukana; Na aibu yako isiondoke. Neno linenwalo wakati wa kufaa, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha. Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo. Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao. Kama mawingu na upepo pasipo mvua; Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo. Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa. Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha; Usije ukashiba na kuitapika. Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; Asije akakukinai na kukuchukia.
Methali 25:7-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,” kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu. Kile ulichokiona kwa macho yako usiharakishe kukipeleka mahakamani, maana utafanya nini mwishoni kama jirani yako atakuaibisha? Ukifanya shauri na jirani yako, usisaliti siri ya mtu mwingine, ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha, na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka. Neno lisemwalo kwa wakati ufaao ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha. Kama vile kipuli cha dhahabu au pambo la dhahabu safi, ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima kwa sikio lisikilizalo. Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao, huburudisha roho za bwana zake. Kama vile mawingu na upepo pasipo mvua ndivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi. Kwa uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, nao ulimi laini unaweza kuvunja mfupa. Ukipata asali, kula kiasi tu cha kukutosha, ukila zaidi, utatapika. Nenda nyumbani mwa jirani yako mara chache; ukizidisha, atakukinai na atakuchukia.