Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 25

25
KITABU CHA NNE
Mithali nyingine za Sulemani
1Hizi nazo ni mithali za Sulemani, ambazo watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda, walizinakili.
2 # Rum 11:33; Ayu 29:16 Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo;
Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo.
3Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini;
Lakini mioyo ya wafalme haichunguziki.
4Ondoa takataka katika fedha,
Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;
5Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme,
Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki.
6 # Lk 14:8-10 Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme;
Wala usisimame mahali pa watu wakuu;
7Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele;
Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu.
Yale uliyoyaona kwa macho,
8 # Mt 5:25 Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania;
Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye,
Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha.
9 # Mt 18:15 Ujitetee na mwenzako peke yake;
Bali usiifunue siri ya mtu mwingine;
10Yeye asikiaye asije akakutukana;
Na aibu yako isiondoke.
11Neno linenwalo wakati ufaao,
Ni kama machungwa katika vyano vya fedha.
12Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi;
Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
13Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno;
Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao;
Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
14 # Yud 1:12 Kama mawingu na upepo pasipo mvua;
Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo.
15Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa;
Na ulimi laini huvunja mfupa.
16Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha;
Usije ukashiba na kuitapika.
17Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi;
Asije akakukinai na kukuchukia.
18 # Zab 140:3 Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo
Ni nyundo, na upanga, na mshale mkali.
19 # Ayu 6:14-20; 2 Tim 4:16 Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu
Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.
20 # Dan 6:18 Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito,
Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi;
Ni kama siki juu ya magadi.
21 # Rum 12:20; Mt 5:44 Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula;
Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa;
22 # 2 Sam 16:12 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake;
Na BWANA atakupa thawabu.
23Upepo wa kusi huleta mvua;
Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.
24Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini,
Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
25Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu,
Ndivyo ilivyo habari njema itokayo katika nchi ya mbali.
26 # Mik 7:8 Mwenye haki amwangukiapo mtu mbaya
Ni kama chemchemi iliyochafuka,
Na kisima kilichokanyagwa.
27 # Lk 14:11 Haifai kula asali nyingi mno;
Vile vile mtu kutafuta utukufu wake mwenyewe si utukufu.
28Asiyetawala roho yake
Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta.

Iliyochaguliwa sasa

Mithali 25: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha