Methali 21:8-10
Methali 21:8-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Njia ya mtu mwenye hatia imepotoka, lakini mwenendo wa mnyofu umenyooka. Afadhali kuishi pembeni juu ya paa, kuliko kuishi nyumbani na mwanamke mgomvi. Anachopania kutenda mtu mbaya ni uovu; hata kwa jirani yake hana huruma.
Methali 21:8-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana; Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa. Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi. Nafsi ya mtu mbaya hutamani uovu; Jirani yake hapati fadhili machoni pake.
Methali 21:8-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana; Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa. Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi. Nafsi ya mtu mbaya hutamani uovu; Jirani yake hapati fadhili machoni pake.
Methali 21:8-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu, bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu. Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi. Mtu mwovu hutamani sana ubaya, jirani yake hapati huruma kutoka kwake.