Methali 20:4-6
Methali 20:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mvivu halimi wakati wa kulima; wakati wa mavuno atatafuta asipate chochote. Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji; lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo. Watu wengi hujivunia kuwa wema, lakini mwaminifu wa kweli apatikana wapi?
Methali 20:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu. Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka. Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
Methali 20:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu. Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka. Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
Methali 20:4-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mvivu halimi kwa majira; kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama lakini hapati chochote. Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina, lakini mtu mwenye ufahamu huyachota. Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma, bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?