Methali 2:6-10
Methali 2:6-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Huwawekea wanyofu akiba ya hekima safi, yeye ni ngao kwa watu waishio kwa uaminifu. Huilinda mienendo ya watu watendao haki, na kuzihifadhi njia za waaminifu wake. Ukinisikiliza utafahamu uadilifu na haki, utajua jambo lililo sawa na jema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, na maarifa yataipendeza nafsi yako.
Methali 2:6-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako
Methali 2:6-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako
Methali 2:6-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa maana BWANA hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama, kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu wake. Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki, na sawa: yaani kila njia nzuri. Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.