Methali 2:11-15
Methali 2:11-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Busara itakulinda, ufahamu utakuhifadhi; vitakuepusha na njia ya uovu, na watu wa maneno mapotovu; watu waziachao njia nyofu, ili kuziendea njia za giza; watu wafurahiao kutenda maovu, na kupendezwa na upotovu wa maovu; watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki.
Methali 2:11-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi. Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka; Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza; Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotovu wa waovu; Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.
Methali 2:11-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi. Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka; Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza; Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotoe wa waovu; Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.
Methali 2:11-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda. Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu, kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka, wale waachao mapito yaliyonyooka wakatembea katika njia za giza, wale wapendao kutenda mabaya na kufurahia upotovu wa ubaya, ambao mapito yao yamepotoka na ambao ni wapotovu katika njia zao.