Methali 2:1-4
Methali 2:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika
Methali 2:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanangu, ukiyakubali maneno yangu, na kuyathamini maagizo yangu; ukitega sikio lako kusikiliza hekima, na kuuelekeza moyo wako upate ufahamu; naam, ukiomba upewe busara, ukisihi upewe ufahamu; ukiitafuta hekima kama fedha, na kuitaka kama hazina iliyofichika
Methali 2:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika
Methali 2:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika
Methali 2:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako, kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu, na kama utaiita busara, na kuita kwa sauti upate ufahamu, na ukiitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa