Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 2:1-22

Methali 2:1-22 Biblia Habari Njema (BHN)

Mwanangu, ukiyakubali maneno yangu, na kuyathamini maagizo yangu; ukitega sikio lako kusikiliza hekima, na kuuelekeza moyo wako upate ufahamu; naam, ukiomba upewe busara, ukisihi upewe ufahamu; ukiitafuta hekima kama fedha, na kuitaka kama hazina iliyofichika; hapo utaelewa ni nini kumcha Mwenyezi-Mungu, utafahamu maana ya kumjua Mungu. Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Huwawekea wanyofu akiba ya hekima safi, yeye ni ngao kwa watu waishio kwa uaminifu. Huilinda mienendo ya watu watendao haki, na kuzihifadhi njia za waaminifu wake. Ukinisikiliza utafahamu uadilifu na haki, utajua jambo lililo sawa na jema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, na maarifa yataipendeza nafsi yako. Busara itakulinda, ufahamu utakuhifadhi; vitakuepusha na njia ya uovu, na watu wa maneno mapotovu; watu waziachao njia nyofu, ili kuziendea njia za giza; watu wafurahiao kutenda maovu, na kupendezwa na upotovu wa maovu; watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki. Hekima itakuwezesha kumkwepa mwanamke mwasherati, mwanamke malaya wa maneno matamu; mwanamke amwachaye mwenzi wa ujana wake, na kulisahau agano la Mungu wake. Nyumba yake yaelekea kuzimu, njia zake zinakwenda ahera. Yeyote amwendeaye kamwe harudi, wala hairudii tena njia ya uhai. Kwa hiyo utafuata mfano wa watu wema, na kuzingatia mienendo ya waadilifu. Maana wanyofu wataipata nchi, na waaminifu watadumu ndani yake. Lakini waovu wataondolewa nchini, na wenye hila watangolewa humo.

Shirikisha
Soma Methali 2

Methali 2:1-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako; Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi. Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka; Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza; Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotovu wa waovu; Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao. Ili kuokoka na malaya, Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake; Amwachaye rafiki wa ujana wake, Na kulisahau agano la Mungu wake. Maana nyumba yake inaelekea mauti, Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu. Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja, Wala hawazifikilii njia za uzima. Ili upate kwenda katika njia ya watu wema, Na kuyashika mapito ya wenye haki. Maana wanyofu watakaa katika nchi, Na wakamilifu watadumu ndani yake. Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang'olewa.

Shirikisha
Soma Methali 2

Methali 2:1-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako; Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi. Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka; Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza; Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotoe wa waovu; Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao. Ili kuokoka na malaya, Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake; Amwachaye rafiki wa ujana wake, Na kulisahau agano la Mungu wake. Maana nyumba yake inaelekea mauti, Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu. Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja, Wala hawazifikilii njia za uzima. Ili upate kwenda katika njia ya watu wema, Na kuyashika mapito ya wenye haki. Maana wanyofu watakaa katika nchi, Na wakamilifu watadumu ndani yake. Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang’olewa.

Shirikisha
Soma Methali 2

Methali 2:1-22 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako, kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu, na kama utaiita busara, na kuita kwa sauti upate ufahamu, na ukiitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, ndipo utakapoelewa kumcha BWANA na kupata maarifa ya Mungu. Kwa maana BWANA hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama, kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu wake. Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki, na sawa: yaani kila njia nzuri. Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako. Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda. Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu, kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka, wale wanaoacha mapito ya unyoofu, wakatembea katika njia za giza, wale wanaopenda kutenda mabaya, na kufurahia upotovu wa ubaya, ambao mapito yao yamepotoka, na ambao ni wapotovu katika njia zao. Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba, kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno ya kushawishi kutenda ubaya, aliyemwacha mwenzi wa ujana wake na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu. Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo na mapito yake kwenye roho za waliokufa. Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, au kufikia mapito ya uzima. Hivyo utatembea katika njia za watu wema na kushikamana na mapito ya wenye haki. Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, nao wasio na lawama watabakia ndani yake. Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi, nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo.

Shirikisha
Soma Methali 2