Methali 2:1-15
Methali 2:1-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanangu, ukiyakubali maneno yangu, na kuyathamini maagizo yangu; ukitega sikio lako kusikiliza hekima, na kuuelekeza moyo wako upate ufahamu; naam, ukiomba upewe busara, ukisihi upewe ufahamu; ukiitafuta hekima kama fedha, na kuitaka kama hazina iliyofichika; hapo utaelewa ni nini kumcha Mwenyezi-Mungu, utafahamu maana ya kumjua Mungu. Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Huwawekea wanyofu akiba ya hekima safi, yeye ni ngao kwa watu waishio kwa uaminifu. Huilinda mienendo ya watu watendao haki, na kuzihifadhi njia za waaminifu wake. Ukinisikiliza utafahamu uadilifu na haki, utajua jambo lililo sawa na jema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, na maarifa yataipendeza nafsi yako. Busara itakulinda, ufahamu utakuhifadhi; vitakuepusha na njia ya uovu, na watu wa maneno mapotovu; watu waziachao njia nyofu, ili kuziendea njia za giza; watu wafurahiao kutenda maovu, na kupendezwa na upotovu wa maovu; watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki.
Methali 2:1-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako; Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi. Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka; Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza; Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotovu wa waovu; Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.
Methali 2:1-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako; Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi. Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka; Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza; Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotoe wa waovu; Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.
Methali 2:1-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako, kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu, na kama utaiita busara, na kuita kwa sauti upate ufahamu, na ukiitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, ndipo utakapoelewa kumcha BWANA na kupata maarifa ya Mungu. Kwa maana BWANA hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama, kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu wake. Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki, na sawa: yaani kila njia nzuri. Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako. Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda. Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu, kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka, wale wanaoacha mapito ya unyoofu, wakatembea katika njia za giza, wale wanaopenda kutenda mabaya, na kufurahia upotovu wa ubaya, ambao mapito yao yamepotoka, na ambao ni wapotovu katika njia zao.