Methali 19:3-12
Methali 19:3-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtu akijiangamiza kwa upumbavu wake, huielekeza hasira yake dhidi ya Mwenyezi-Mungu. Mali huvuta marafiki wengi wapya, lakini maskini huachwa bila rafiki. Shahidi mwongo hataacha kuadhibiwa; asemaye uongo hataepa adhabu. Watu wengi hujipendekeza kwa wakuu; kila mtu hutaka kuwa rafiki ya mtu mkarimu. Maskini huchukiwa na ndugu zake; marafiki zake ndio zaidi: Humkimbia! Hata awabembeleze namna gani hatawapata. Ajipatiaye hekima anaipenda nafsi yake; anayezingatia busara atastawi. Shahidi mwongo hatakosa kuadhibiwa; asemaye uongo ataangamia. Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa, tena ni vibaya zaidi mtumwa kuwatawala wakuu. Mwenye busara hakasiriki upesi; kusamehe makosa ni fahari kwake. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba, lakini wema wake ni kama umande juu ya majani.
Methali 19:3-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA. Utajiri huongeza marafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka. Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili; Na kila mtu ni rafiki yake atoaye zawadi. Ndugu zote wa maskini humchukia; Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye! Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka. Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Naye asemaye uongo ataangamia. Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
Methali 19:3-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA. Utajiri huongeza rafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka. Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili; Na kila mtu ni rafiki yake atoaye tunu. Ndugu zote wa maskini humchukia; Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye! Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka. Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Naye asemaye uongo ataangamia. Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
Methali 19:3-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake hata hivyo moyo wake humkasirikia BWANA. Mali huleta rafiki wengi, bali rafiki wa mtu maskini humwacha. Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo hataachwa huru. Wengi hujipendekeza kwa mtawala na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi. Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote: Je, rafiki zake watamkwepa kiasi gani! Ingawa huwafuata kwa kuwasihi, hawapatikani popote. Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, yeye ahifadhiye ufahamu hustawi. Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo ataangamia. Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, itakuwa vibaya kiasi gani kwa mtumwa kuwatawala wakuu. Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi.