Methali 19:1-3
Methali 19:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Afadhali maskini aishiye kwa unyofu, kuliko mtu mpotovu wa maneno na mpumbavu. Haifai mtu kuwa bila akili; mwenda harakaharaka hujikwaa. Mtu akijiangamiza kwa upumbavu wake, huielekeza hasira yake dhidi ya Mwenyezi-Mungu.
Methali 19:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Afadhali maskini aendaye katika uadilifu wake, Kuliko mpotovu wa midomo aliye mpumbavu. Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi. Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA.
Methali 19:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa midomo aliye mpumbavu. Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi. Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA.
Methali 19:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka. Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, wala kufanya haraka na kuikosa njia. Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake hata hivyo moyo wake humkasirikia BWANA.