Methali 16:6-9
Methali 16:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa utii na uaminifu mtu huondolewa dhambi, kwa kumcha Mwenyezi-Mungu huepuka uovu. Mwenyezi-Mungu akipendezwa na mwenendo wa mtu, huwageuza hata adui zake kuwa marafiki. Afadhali mali kidogo kwa uadilifu, kuliko mapato mengi kwa udhalimu. Mtu aweza kufanya mipango yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake.
Methali 16:6-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye. Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.
Methali 16:6-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye. Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.
Methali 16:6-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha BWANA mtu hujiepusha na ubaya. Njia za mtu zinapompendeza BWANA, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani. Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali BWANA huelekeza hatua zake.