Methali 16:3-9
Methali 16:3-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake; hata waovu kwa ajili ya siku ya maangamizi. Kila mwenye kiburi ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; hakika mtu wa namna hiyo hataacha kuadhibiwa. Kwa utii na uaminifu mtu huondolewa dhambi, kwa kumcha Mwenyezi-Mungu huepuka uovu. Mwenyezi-Mungu akipendezwa na mwenendo wa mtu, huwageuza hata adui zake kuwa marafiki. Afadhali mali kidogo kwa uadilifu, kuliko mapato mengi kwa udhalimu. Mtu aweza kufanya mipango yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake.
Methali 16:3-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye. Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.
Methali 16:3-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye. Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.
Methali 16:3-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mkabidhi BWANA lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. BWANA hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi. BWANA huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa. Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha BWANA mtu hujiepusha na ubaya. Njia za mtu zinapompendeza BWANA, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani. Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali BWANA huelekeza hatua zake.