Methali 16:21-23
Methali 16:21-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenye hekima moyoni huitwa mwenye akili; neno la kupendeza huwavutia watu. Hekima ni chemchemi ya uhai kwake aliye nayo, bali upumbavu ni adhabu ya wapumbavu. Moyo wa mwenye hekima humwezesha kusema kwa busara; huyafanya maneno yake yawe ya kuvutia.
Methali 16:21-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu. Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao. Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake.
Methali 16:21-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu. Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao. Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake.
Methali 16:21-23 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu, na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho. Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao, bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu. Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho.