Methali 16:17-19
Methali 16:17-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Njia ya wanyofu huepukana na uovu; anayechunga njia yake huhifadhi maisha yake. Kiburi hutangulia maangamizi; majivuno hutangulia maanguko. Afadhali kuwa mnyenyekevu na kuwa maskini, kuliko kugawana nyara na wenye kiburi.
Methali 16:17-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake. Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.
Methali 16:17-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake. Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.
Methali 16:17-19 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya; yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake. Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko. Ni afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu miongoni mwa walioteswa kuliko kugawana nyara na wenye kiburi.