Methali 13:2-3
Methali 13:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtu mwema hupata mema kutokana na maneno yake, lakini wadanganyifu huishi kwa ukatili. Achungaye mdomo wake huyahifadhi maisha yake, anayeropoka ovyo hujiletea maangamizi.
Shirikisha
Soma Methali 13Methali 13:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri. Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.
Shirikisha
Soma Methali 13Methali 13:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri. Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.
Shirikisha
Soma Methali 13