Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wafilipi 2:9-11 - Compare All Versions

Wafilipi 2:9-11 BHN (Biblia Habari Njema)

Kwa sababu hiyo Mungu alimkweza juu kabisa, akampa jina lililo kuu kuliko majina yote. Ili kwa heshima ya jina la Yesu, viumbe vyote mbinguni, duniani na kuzimu, vipige magoti mbele yake, na kila mtu akiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Shirikisha
Wafilipi 2 BHN

Wafilipi 2:9-11 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Shirikisha
Wafilipi 2 SRUV

Wafilipi 2:9-11 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Shirikisha
Wafilipi 2 SUV

Wafilipi 2:9-11 NEN (Neno)

Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana, na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina, ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Shirikisha
Wafilipi 2 NEN