Wafilipi 1:1-2
Wafilipi 1:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi Paulo na Timotheo, watumishi wa Yesu Kristo, tunawaandikia nyinyi watu wa Mungu huko Filipi ambao mmeunganishwa na Kristo Yesu, pamoja na viongozi na wasaidizi wa kanisa. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
Shirikisha
Soma Wafilipi 1Wafilipi 1:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo Yesu, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na maaskofu na mashemasi. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Shirikisha
Soma Wafilipi 1Wafilipi 1:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo Yesu, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na maaskofu na mashemasi. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Shirikisha
Soma Wafilipi 1