Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 29:1-11

Hesabu 29:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

“Siku ya kwanza ya mwezi wa saba, mtafanya mkutano mtakatifu. Msifanye kazi. Hiyo ni siku ya kupiga tarumbeta. Mtatoa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali wachanga wawili, kondoo madume wawili, na wanakondoo wa kiume saba wa mwaka mmoja, wote wawe wasio na dosari yoyote. Mtatoa pia sadaka yake ya nafaka ya unga safi uliochanganywa na mafuta: Kilo tatu kwa kila fahali, kilo mbili kwa kila kondoo dume, na kilo moja kwa kila mwanakondoo. Tena mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi ili kuwafanyia upatanisho. Mtatoa vitu hivi licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya mwezi mpya na sadaka yake ya nafaka, na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji kama inavyotakiwa kuwa harufu nzuri ipendezayo, ni sadaka kwa Mwenyezi-Mungu iliyoteketezwa kwa moto. “Siku ya kumi ya mwezi wa saba mtafanya mkutano mtakatifu. Siku hiyo ni lazima mfunge na msifanye kazi. Mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu: Fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, wanakondoo saba wa mwaka mmoja. Wote wasiwe na dosari. Licha ya vitu hivi mtatoa sadaka ya unga safi uliochanganywa na mafuta kilo tatu pamoja na huyo fahali, kilo mbili pamoja na yule kondoo dume, na kilo moja kwa kila mwanakondoo. Mtatoa pia beberu mmoja kwa sadaka ya kuondoa dhambi licha ya sadaka ya kufanyiwa upatanisho, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka na sadaka zake za kinywaji.

Shirikisha
Soma Hesabu 29

Hesabu 29:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Tena mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote ya utumishi; ni siku ya kupiga tarumbeta kwenu. Nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja wote wasiwe na dosari; pamoja na sadaka yake ya unga, unga laini uliochanganywa na mafuta, sehemu ya tatu ya kumi ya ng'ombe, sehemu ya mbili ya kumi kwa kondoo dume, na sehemu ya moja ya kumi kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto. Tena siku ya kumi ya huo mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; nanyi mtajinyima nafsi zenu, msifanye kazi yoyote ya utumishi lakini mtamsogezea BWANA sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja; watakuwa wakamilifu kwenu; pamoja na sadaka zake za unga, unga laini uliochanganywa na mafuta, sehemu ya tatu ya kumi kwa huyo ng'ombe, na sehemu ya mbili ya kumi kwa huyo kondoo, na sehemu ya moja ya kumi kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.

Shirikisha
Soma Hesabu 29

Hesabu 29:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Tena mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; ni siku ya kupiga tarumbeta kwenu. Nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng’ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba; pamoja na sadaka yake ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa ng’ombe, sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume, na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto. Tena siku ya kumi ya huo mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; nanyi mtazitesa nafsi zenu, msifanye kazi yo yote ya utumishi lakini mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng’ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu; pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa huyo ng’ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa huyo kondoo, na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.

Shirikisha
Soma Hesabu 29

Hesabu 29:1-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

“ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta. Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayo BWANA ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume, andaa unga sehemu mbili za kumi ya efa; na pamoja na wana-kondoo saba kila mmoja aandaliwe na sehemu ya kumi ya efa ya unga. Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku, pamoja na sadaka zake za nafaka, na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwa BWANA kwa moto, harufu inayopendeza. “ ‘Kwenye siku ya kumi ya mwezi huu wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu. Mtajikana wenyewe na msifanye kazi. Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza BWANA. Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, sehemu mbili za kumi ya efa ya unga laini; na kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba andaa sehemu ya kumi ya unga laini kwa kila mmoja. Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.

Shirikisha
Soma Hesabu 29