Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 26:1-51

Hesabu 26:1-51 Biblia Habari Njema (BHN)

Baada ya yale maradhi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni, “Hesabuni jumuiya yote ya Waisraeli, kila mtu kufuatana na jamaa yake. Wahesabuni watu wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi wanaofaa kwenda jeshini.” Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko, wakawaambia, “Hesabuni watu kuanzia na wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.” Idadi ya Waisraeli waliotoka Misri ni hii: Kwanza ni kabila la Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. Henoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hizo ndizo koo za kabila la Reubeni. Idadi ya wanaume waliohesabiwa ni 43,730. Wazawa wa Palu walikuwa Eliabu, na wanawe Nemueli, Dathani na Abiramu. (Hawa wawili: Dathani na Abiramu, ndio waliokuwa wamechaguliwa miongoni mwa jumuiya, lakini wakampinga Mose na Aroni, na kujiunga na wafuasi wa Kora wakati walipomwasi Mwenyezi-Mungu. Wakati huo ardhi ilifunguka ikawameza, wakafa pamoja na Kora na wafuasi wake moto ulipoangamiza watu 250; wakawa onyo kwa watu. Pamoja na hayo wana wa Kora hawakufa.) Kabila la Simeoni. Nemueli, Yamini, Yakini, Zera na Shauli. Hizo ndizo koo za kabila la Simeoni, jumla yao wanaume 22,000. Kabila la Gadi lilikuwa na jamaa za Sefoni, Hagi, Shuni, Ozni, Eri, Arodi na Areli. Hizo ndizo koo za kabila la Gadi, jumla wanaume 40,500. Kabila la Yuda lilikuwa na wanawe wa Yuda Eri na Onani. Hawa walifia nchini Kanaani. Kabila la Yuda lilikuwa na jamaa za Shela, Peresi, na Zera. Kutoka kwa Peresi, familia ya Hesroni na Hamuli. Hizo ndizo koo za Yuda, jumla wanaume 76,500. Kabila la Isakari lilikuwa na jamaa za Tola, Puva, Yashubu na wa Shimroni. Hizo ndizo koo za Isakari, jumla wanaume 64,300. Kabila la Zebuluni lilikuwa na jamaa za Seredi, wa Eloni na wa Yaleeli. Hizo ndizo koo za Zebuluni, jumla wanaume 60,500. Kabila la Yosefu baba yao Manase na Efraimu. Kabila la Manase lilikuwa na jamaa ya: Makiri, Gileadi. Yezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Shemida na Heferi. Selofehadi, mwana wa Heferi hakupata watoto wa kiume bali wa kike tu, nao ni Mala, Noa, Hogla, Milka na Tirza. Hizo ndizo koo za Manase, jumla wanaume 52,700. Kabila la Efraimu lilikuwa na jamaa za Shuthela, Bekeri na Tahani. Ukoo wa Erani ulikuwa na jamaa ya Shuthela. Hizo ndizo koo za Efraimu, jumla wanaume 32,500. Zote hizo zilitokana na Yosefu. Kabila la Benyamini lilikuwa na jamaa za Bela, Ashbeli, Ahiramu, Shufamu na Hufamu. Koo za Ardi na Naamani, zilitokana na Bela. Hizo ndizo koo za Benyamini, jumla wanaume 45,600. Kabila la Dani lilikuwa na jamaa ya Shuhamu; ukoo ulikuwa na wanaume 64,400. Kabila la Asheri lilikuwa na jamaa za Imna, Ishvi na Beria. Koo za Heberi na Malkieli zilitokana na Beria. Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera. Hizo ndizo koo za kabila la Asheri, jumla wanaume 53,400. Kabila la Naftali lilikuwa na jamaa za Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu. Hizi ndizo koo za kabila la Naftali, jumla wanaume 45,400. Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730.

Shirikisha
Soma Hesabu 26

Hesabu 26:1-51 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Ikawa baada ya hilo pigo, BWANA akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia, Fanya hesabu ya jumuiya yote ya wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani. Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia, Fanyeni hesabu ya watu, kuanzia umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama BWANA alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri. Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu; na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi. Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tatu, mia saba na thelathini. Na wana wa Palu; Eliabu. Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na BWANA; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara. Hata hivyo, hao wana wa Kora hawakufa. Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini; wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli. Hawa ndizo jamaa wa Wasimeoni, watu elfu ishirini na mbili na mia mbili. Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni; wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri; wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli. Hawa ndio jamaa wa wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, elfu arubaini na mia tano. Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera. Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli. Hawa ndio jamaa wa Yuda kama waliohesabiwa kwao, elfu sabini na sita na mia tano. Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva; wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni. Hawa ndio jamaa wa Isakari kama waliohesabiwa kwao, elfu sitini na nne na mia tatu. Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli. Hawa ndio jamaa wa Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, elfu sitini na mia tano. Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu. Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi. Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki; na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu; na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi. Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na watoto wa kiume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Nuhu, na Hogla, na Milka, na Tirza. Hawa ndizo jamaa wa Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni elfu hamsini na mbili na mia saba. Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi. Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani. Hawa ndio jamaa wa wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, elfu thelathini na mbili na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao. Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu; wa Shufamu, jamaa ya Washufamu; wa Hufamu, jamaa ya Wahufamu. Na wana wa Bela walikuwa Ardi na Naamani; wa Ardi, jamaa ya Waardi; wa Naamani, jamaa ya Wanaamani. Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia sita. Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao. Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sitini na nne na mia nne. Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia. Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli. Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera. Hawa ndio jamaa wa wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, elfu hamsini na tatu na mia nne. Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni; wa Yeseri, jamaa ya Wayeseri, wa Shilemu jamaa ya Washilemu. Hawa ndio jamaa wa Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia nne. Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, elfu mia sita na moja, mia saba na thelathini (601,730).

Shirikisha
Soma Hesabu 26

Hesabu 26:1-51 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Ikawa baada ya hilo pigo, BWANA akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia, Fanya jumla ya mkutano wote wa wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani. Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia, Fanyeni jumla ya watu, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama BWANA alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri. Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu; na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi. Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tatu elfu na mia saba na thelathini. Na wana wa Palu; Eliabu. Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na BWANA; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara. Pamoja na hayo, hao wana wa Kora hawakufa. Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini; wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli. Hizi ndizo jamaa za Wasimeoni, watu ishirini na mbili elfu na mia mbili. Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni; wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri; wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli. Hizi ndizo jamaa za wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, arobaini elfu na mia tano. Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera. Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli. Hizi ndizo jamaa za Yuda kama waliohesabiwa kwao, sabini na sita elfu na mia tano. Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva; wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni. Hizi ndizo jamaa za Isakari kama waliohesabiwa kwao, sitini na nne elfu na mia tatu. Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli. Hizi ndizo jamaa za Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, sitini elfu na mia tano. Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu. Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi. Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki; na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu; na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi. Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na wana waume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa. Hizi ndizo jamaa za Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni hamsini na mbili elfu na mia saba. Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi. Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani. Hizi ndizo jamaa za wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, thelathini na mbili elfu na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao. Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu; wa Shufamu, jamaa ya Washufamu; wa Hufamu, jamaa ya Wahufamu. Na wana wa Bela walikuwa Ardi na Naamani; wa Ardi, jamaa ya Waardi; wa Naamani, jamaa ya Wanaamani. Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia sita. Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao. Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa sitini na nne elfu na mia nne. Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia. Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli. Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera. Hizi ndizo jamaa za wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, hamsini na tatu elfu na mia nne. Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni; wa Yeseri, jamaa ya Wayeseri, wa Shilemu jamaa ya Washilemu. Hizi ndizo jamaa za Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia nne. Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, mia sita na moja elfu, na mia saba na thelathini (601,730).

Shirikisha
Soma Hesabu 26

Hesabu 26:1-51 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Baada ya hiyo tauni, BWANA akamwambia Musa na Eleazari mwana wa kuhani Haruni, “Hesabu jumuiya yote ya Waisraeli kufuatana na jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, wanaoweza kutumika katika jeshi la Israeli.” Hivyo Musa na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ngʼambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema, “Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama BWANA alivyomwagiza Musa.” Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri: Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa: kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki; kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu; kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi. Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa elfu arobaini na tatu mia saba na thelathini (43,730). Mwana wa Palu alikuwa Eliabu, nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Musa na Haruni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi BWANA. Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume mia mbili na hamsini. Nao walikuwa kama alama ya onyo. Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa. Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli; kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini; kutoka wa Yakini, ukoo wa Wayakini; kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera; kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli. Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia mbili. Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni; kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi; kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni; kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni; kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri; kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi; kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli. Hizo zilikuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa elfu arobaini na mia tano. Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani. Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela; kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi; kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera. Wazao wa Peresi walikuwa: kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli. Hizo zilikuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa elfu sabini na sita na mia tano. Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola; kutoka kwa Puva, ukoo wa Wapuva; kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu; kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni. Hizo zilikuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa elfu sitini na nne na mia tatu. Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi; kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni; kutoka kwa Yaleeli, ukoo wa Wayaleeli. Hizo zilikuwa koo za Zabuloni; wale waliohesabiwa walikuwa elfu sitini na mia tano. Wazao wa Yusufu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa: Wazao wa Manase: kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi); kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi. Hawa walikuwa wazao wa Gileadi: kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri; kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki; kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli; kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu; kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida; kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi. (Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.) Hizo zilikuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa elfu hamsini na mbili na mia saba. Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao: kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela; kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri; kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani; Hawa walikuwa wazao wa Shuthela: kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani. Hizo zilikuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa elfu thelathini na mbili na mia tano. Hao walikuwa wazao wa Yusufu kwa koo zao. Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela; kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli; kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu; kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu; kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu. Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa: kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi; kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani. Hizo zilikuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa elfu arobaini na tano na mia sita. Hawa walikuwa wazao wa Dani kwa koo zao: kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizo zilikuwa koo za Dani: Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa elfu sitini na nne na mia nne. Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna; kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi; kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia; kutoka kwa wazao wa Beria: kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi; kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli. Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera. Hizo zilikuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa elfu hamsini na tatu na mia nne. Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Yaseeli, ukoo wa Wayaseeli; kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni; kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri; kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu. Hizo zilikuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa elfu arobaini na tano na mia nne. Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa elfu mia sita na moja mia saba na thelathini (601,730).

Shirikisha
Soma Hesabu 26