Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 26

26
Kuhesabu watu mara ya pili
1Baada ya hiyo tauni, Bwana akamwambia Musa na Eleazari mwana wa kuhani Haruni, 2“Hesabu jumuiya yote ya Waisraeli kufuatana na jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, wanaoweza kutumika katika jeshi la Israeli.” 3Hivyo Musa na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ngʼambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema, 4“Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Musa.”
Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri:
5Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa:
kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki;
kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;
6kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;
kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.
7Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa elfu arobaini na tatu mia saba na thelathini (43,730).
8Mwana wa Palu alikuwa Eliabu, 9nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Musa na Haruni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi Bwana. 10Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume mia mbili na hamsini. Nao walikuwa kama alama ya onyo. 11Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.
12Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli;
kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini;
kutoka wa Yakini, ukoo wa Wayakini;
13kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera;
kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli.
14Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia mbili.
15Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni;
kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi;
kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;
16kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni;
kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri;
17kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi;
kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli.
18Hizo zilikuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa elfu arobaini na mia tano.
19Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.
20Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela;
kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi;
kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera.
21Wazao wa Peresi walikuwa:
kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;
kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.
22Hizo zilikuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa elfu sabini na sita na mia tano.
23Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola;
kutoka kwa Puva, ukoo wa Wapuva;
24kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu;
kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.
25Hizo zilikuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa elfu sitini na nne na mia tatu.
26Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi;
kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni;
kutoka kwa Yaleeli, ukoo wa Wayaleeli.
27Hizo zilikuwa koo za Zabuloni; wale waliohesabiwa walikuwa elfu sitini na mia tano.
28Wazao wa Yusufu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:
29Wazao wa Manase:
kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi);
kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi.
30Hawa walikuwa wazao wa Gileadi:
kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri;
kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki;
31kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli;
kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu;
32kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida;
kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi.
33(Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.)
34Hizo zilikuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa elfu hamsini na mbili na mia saba.
35Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao:
kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela;
kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri;
kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani;
36Hawa walikuwa wazao wa Shuthela:
kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani.
37Hizo zilikuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa elfu thelathini na mbili na mia tano.
Hao walikuwa wazao wa Yusufu kwa koo zao.
38Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela;
kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli;
kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu;
39kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu;
kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.
40Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa:
kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi;
kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani.
41Hizo zilikuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa elfu arobaini na tano na mia sita.
42Hawa walikuwa wazao wa Dani kwa koo zao:
kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu.
Hizo zilikuwa koo za Dani: 43Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa elfu sitini na nne na mia nne.
44Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna;
kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi;
kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;
45kutoka kwa wazao wa Beria:
kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi;
kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli.
46Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.
47Hizo zilikuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa elfu hamsini na tatu na mia nne.
48Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa:
kutoka kwa Yaseeli, ukoo wa Wayaseeli;
kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni;
49kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri;
kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.
50Hizo zilikuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa elfu arobaini na tano na mia nne.
51Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa elfu mia sita na moja mia saba na thelathini (601,730).
52 Bwana akamwambia Musa, 53“Watagawiwa nchi kama urithi kulingana na hesabu ya majina. 54Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa. 55Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao. 56Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”
57Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao:
kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagershoni;
kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi;
kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari.
58Hizi pia zilikuwa koo za Walawi:
ukoo wa Walibni;
ukoo wa Wahebroni;
ukoo wa Wamahli;
ukoo wa Wamushi;
ukoo wa wana wa Kora.
(Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu; 59jina la mke wa Amramu ni Yokebedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Haruni, Musa na dada yao Miriamu. 60Haruni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari. 61Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walitoa sadaka mbele za Bwana kwa moto usioruhusiwa.)
62Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa elfu ishirini na tatu. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.
63Hawa ndio walioorodheshwa na Musa na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani, ngʼambo ya Yeriko. 64Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Musa na kuhani Haruni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai. 65Kwa maana Bwana alikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 26: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia