Hesabu 22:20-21
Hesabu 22:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, Mungu akamjia Balaamu usiku huo, akamwambia, “Kama watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao, lakini fanya tu kile nitakachokuambia.” Balaamu akaamka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na hao maofisa.
Hesabu 22:20-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi. Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu.
Hesabu 22:20-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, enenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi. Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu.