Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 22

22
Balaki amwita Balaamu na awalaani Waisraeli
1 # Hes 33:48; Mwa 35:5; Kut 23:27; Kum 2:25; Yos 2:9; Yer 32:21 Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu na Yeriko. 2#Amu 11:25 Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori. 3#Kut 15:15 Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli. 4#Hes 31:8; Yos 13:21 Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile. 5#Hes 31:8; 2 Pet 2:15-16; Yud 11; Kum 23:4; Yos 13:22; Neh 13:1,2; Mik 6:5 Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hadi Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi. 6#Mwa 12:3; 27:29; Hes 23:7; Kum 23:4; Yos 24:9; 1 Sam 17:43; Neh 13:2 Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa. 7#Kut 23:8; 1 Sam 9:7,8; Mit 17:23; Isa 56:11; Mik 3:11 Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki. 8Akawaambia, Kaeni hapa usiku huu, nami nitawaletea jawabu kama BWANA atakavyoniambia; wakuu wa Moabu wakakaa na Balaamu. 9#Mwa 20:3; 31:24 Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe? 10Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema, 11Tazama, kuna watu waliotoka Misri, wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa; labda nitaweza kupigana nao, na kuwafukuza. 12#Mwa 12:2; 22:17; 28:13,14; Hes 23:20; Kum 23:5; 33:29; Zab 144:15; Rum 11:29 Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa. 13Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Nendeni zenu hadi nchi yenu; kwa maana BWANA amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi. 14Wakuu wakaondoka wakaenda kwa Balaki, wakasema, Balaamu, anakataa kuja pamoja nasi.
15Basi Balaki akatuma wakuu mara ya pili, wengi zaidi, wenye cheo cha juu kuliko wale wa kwanza. 16Wakamfikia Balaamu, wakamwambia, Balaki mwana wa Sipori asema hivi, Nakusihi, neno lolote lisikuzuie usinijie; 17#Kum 16:19; Zab 49:17; Mt 4:8,9; 16:26 maana nitakutunukia heshima kubwa sana, na neno lolote utakaloniomba nitalitenda; basi njoo, nakusihi, unilaanie watu hawa. 18#1 Fal 22:14; 2 Nya 18:13 Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Hata kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la BWANA, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza. 19Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua BWANA atakaloniambia zaidi. 20#Hes 23:12,26; 24:13; Zab 33:10,11; Isa 37:29; 46:10 Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi. 21#Mit 15:27; 1 Tim 6:9,10; 2 Pet 2:15; Yud 1:11 Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu.
Balaamu, punda na malaika
22 # Kut 4:24; 23:20 Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa BWANA akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye. 23#2 Fal 6:17 Na yule punda akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, na upanga wake mkononi mwake amekwisha kuufuta; punda akageuka upande ili kuiacha njia, akaingia shambani. Balaamu akampiga punda ili kumrejesha njiani. 24Kisha malaika wa BWANA akasimama mahali penye bonde, katikati ya mashamba ya mizabibu, tena penye kitalu upande huu na kitalu upande huu. 25#Isa 47:12; 1 Kor 3:19 Yule punda akamwona malaika wa BWANA, akajisukuma ukutani, akaubana mguu wake Balaamu, basi akampiga mara ya pili. 26#Isa 26:11; Hos 2:6 Malaika wa BWANA akaenda mbele akasimama mahali pembamba sana, hapakuwa na nafasi ya kugeukia mkono wa kulia, wala mkono wa kushoto. 27#Mit 14:16; 27:3,4; Yak 1:19 Yule punda akamwona malaika wa BWANA, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake. 28#Mt 19:26; 1 Kor 1:19; 2 Pet 2:16 BWANA akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi? 29#Mit 12:10; Mhu 9:3; Yer 17:9; Mt 15:19 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi. 30#1 Kor 1:27 Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La! 31#Mwa 21:19; 2 Fal 6:17; 1 Nya 21:16; Lk 24:16; Ayu 8:20; Mit 11:2; Yer 3:25 Ndipo BWANA akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, akiwa na upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa, naye akainamisha kichwa, akaanguka kifudifudi. 32#Kum 23:4; Mit 28:6; Mik 6:5; Mdo 13:10; 2 Pet 2:14,15 Malaika wa BWANA akamwambia, Mbona umempiga punda wako mara tatu hizi? Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka#22:32 ‘Au njia yako ni mbaya’. mbele zangu, 33punda akaniona, akageuka upande mbele zangu mara tatu hizi; kama asingejiepusha nami, bila shaka ningalikuua wewe, nikamwacha yeye hai. 34#1 Sam 26:21; 2 Sam 12:13 Balaamu akamwambia malaika wa BWANA, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena. 35Malaika wa BWANA akamwambia Balaamu Nenda pamoja na watu hawa, lakini neno lile nitakalokuambia, ndilo utakalosema. Basi Balaamu akaenda pamoja na wakuu wa Balaki.
36 # Mwa 14:17; 18:2; Kut 18:7; 1 Sam 13:10; Mdo 28:15 Balaki aliposikia ya kuwa Balaamu amefika, akatoka kwenda kumlaki, mpaka Mji wa Moabu, ulioko katika mpaka wa Arnoni, ulioko katika upande wa mwisho wa mpaka huo. 37Balaki akamwambia Balaamu, Je! Mimi sikutuma watu kwako kwa bidii ili kukuita? Mbona hukunijia? Je! Siwezi mimi kukufanyizia heshima nyingi? 38#1 Fal 22:14; 2 Nya 18:13 Balaamu akamwambia Balaki, Tazama, nimekujia. Je! Mimi sasa nina uwezo wowote kusema neno lolote? Neno lile Mungu atakalolitia kinywani mwangu, ndilo nitakalolisema. 39Balaamu akaenda pamoja na Balaki wakafika Kiriath-husothi. 40Balaki akachinja ng'ombe, na kondoo, akampelekea Balaamu na wale wakuu waliokuwa pamoja naye.
Aguzi la kwanza la Balaamu
41 # Kum 12:2; 2 Nya 11:15; Yer 48:35 Ikawa asubuhi Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hadi Bamoth-baali; na kutoka huko aliweza kuwaona baadhi ya Waisraeli#22:41 Katika Kiebrania ni akawaona watu. hadi pande zao za mwisho.

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 22: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha