Mathayo 5:2-6
Mathayo 5:2-6 Biblia Habari Njema (BHN)
naye akaanza kuwafundisha: “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa. Heri walio wapole, maana watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.
Mathayo 5:2-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
Mathayo 5:2-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
Mathayo 5:2-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo akaanza kuwafundisha, akisema: “Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa. Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.